Jukwaa la Wananchi
Register Calendar
 
 
 


Reply
  Author   Comment  
Unregistered
Reply with quote  #1 


IKIWA ni wiki ya lala salama ya kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la uwakilishi la Uzini, visiwani Zanzibar, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) tayari kimefanya mikutano 68 ya kumnadi mgombea wake, Ali Mbarouk Mshimba.

Hatua hiyo inatokana na chama hicho kufanya mikutano minane ya hadhara kila siku ili kuhakikisha jimbo hilo linatua mikononi mwake pamoja na kuwafikia wananchi wengi.

Katika mkutano uliofanyika kwenye Shehia ya Pagali, kada wa CHADEMA, Mtera Mwampamba, aliwataka vijana kujiepusha na kasumba ya kubebwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye mikutano yake kwa ahadi ya kupatiwa ajira.

Mwampamba alisema badala yake vijana hao wanatakiwa kukumbuka walichofanyiwa katika uchaguzi mkuu uliopita baada ya kubebwa na kupelekwa kisiwani Pemba ambapo wengi wao walirudi na vilema na wengine kupoteza maisha.

Aliwataka vijana hao wasiwe na ugonjwa wa kusahau kiasi hicho, kwa kuwa hadi leo kati ya hao waliopelekwa, hakuna hata mmoja aliyepata ajira.

Naye, Ofisa Mwandamizi wa Utafiti na Sera wa CHADEMA, Mwita Waitara, aliwataka wakazi wa Uzini kutosita kuitosa CCM, kwa kuwa katika miaka 48 iliyokaa madarakani hakuna maendeleo iliyowafanyia.

Akitolea mfano alisema Uzini leo isingetakiwa kukosa huduma za maji ukizingatia kwamba Zanzibar pembe zote imezungukwa na maji, pia jimbo hilo halina shule wala zahanati, pamoja na kufahamika kuwa ndilo la pili katika harakati za kuleta mapinduzi.

Source: T/daima 7 Feb 2012
Previous Topic | Next Topic
Print
Reply


Create your own forum with Website Toolbox!