Jukwaa la Wananchi
Register Calendar
 
 
 


Reply
  Author   Comment  
Mkazi
Reply with quote  #1 
18th October 2011
  Wakili asonywa mahakamani, ahofia usalama
                                               

                                               
Mbunge wa Godbless Lema wa Jimbo la Arusha Mjini
                                       

Kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa Godbless Lema wa Jimbo la Arusha Mjini, imeahirishwa hadi Jumatatu ijayo, baada ya mahakama hiyo kushindwa kuwasilisha nyaraka muhimu. 

Akiahirisha kesi hiyo jana, Jaji Aloyce Mujulizi, alisema wakili wa walalamikiwa Method Kimomogoro, aliomba kupewa nakala ya uamuzi mdogo uliotupilia mbali pingamizi lililowekwa dhidi ya kesi hiyo.

 Pia aliomba kupewa nakala ya mwenendo wa shauri hilo, lakini hadi kesi hiyo inatajwa jana asubuhi upande wa walalamikiwa haukuwa umepata nakala hizo. 

“Nathibitisha drafti na nakala ya mwenendo wa shauri la pingamizi ipo kwenye faili nilikabidhiwa leo,” alisema Jaji Mujulizi. 

Katika uamuzi wake wa kuahirisha kesi, Jaji Mujulizi alimwagiza msajili wa mahakama kutoa nakala hizo kwa wadaiwa na wadai kabla ya kuanza kusilikiza kesi hiyo wiki ijayo.

 Pia alimwagiza msajili wa wilaya kutoa taarifa ya shauri hilo kwa mujibu wa sheria na kubandika kwenye ubao wa matangazo mahakamani hapo na  kuomba ukumbi mkubwa wa kusikilizia kesi hiyo kutokana na idadi kubwa ya watu wanaopenda kwenda kusikiliza. 

Maagizo mengine aliyotoa ni kumtaka msajili kuweka utaratibu wa mwenendo wa shauri hilo kusikilizwa kwa vipaza sauti ili kuruhusu watu wengine watakaoshindwa kuingia ndani ya ukumbi waweze kusikiliza. 

Jaji Mujulizi alitoa amri hizo baada ya wakili wa wadai, Alute Mughwai, kuikumbushia mahakama hiyo kuhusu muda uliopangwa kusikiliza kesi hiyo hadi Desemba kuwa ni mdogo.  Kutokana na hali hiyo, aliomba mahakama hiyo iandae utaratibu wa kuomba muda wa nyongeza, kutoa taarifa ya siku ya kesi kwenye ubao wa matangazo, na kesi hiyo isikilizwe kwenye ukumbi mkubwa zaidi. 

“Hiki chumba hakifai kwa usikilizaji wa kesi hii. Tumejazana na hewa haitoshi. Inatakiwa ipande toka chini hadi kichwani,” alisema.

Aliongeza: “Tunahitaji uwanja mpana wa kufanya kazi yetu.”

Pia Wakili Mughwai alilalamikia suala la usalama mahakamani hapo, lakini wakati akitoa ombi hilo, sauti za kumsonya zilisikika kutoka kwa watu waliokuwa wamekaa nyuma yake. 

“Mheshimiwa Jaji, unasikia jinsi ninavyosonywa? Hii inaonyesha wanataka nisiseme. Na huu sio utaratibu wa kuendesha kesi mahakamani,” alisema. 

Hata hivyo, Jaji Mujulizi alisema, “Hawakusonyi wewe, ila wanaisonya mahakama,” na baada ya kusema hivyo watu hao walisikika wakipiga makofi, lakini baadaye Jaji alionya kwamba anayesonya anaidharau mahakama.

 

                               
                                        CHANZO:                                         NIPASHE                                
Previous Topic | Next Topic
Print
Reply


Create your own forum with Website Toolbox!